Main Title

source : Parstoday
Jumatano

10 Julai 2024

15:11:31
1471075

Kikosi cha SEPAH chaangamiza timu ya magaidi kaskazini magharibi mwa Iran

Kikosi cha nchi kavu cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (SEPAH) kimetangaza kuiangamiza timu ya kigaidi dhidi ya mapinduzi kaskazini magharibi mwa nchi.

Taarifa ya SEPAH imesema, baada ya uchunguzi makini askari wa kambi ya Hamza Sayyid al-Shuhada ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, timu ya kigaidi ya kupambana na mapinduzi iliyokuwa ikipanga kuingia katika ardhi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kutoka kwenye mipaka ya kaskazini magharibi mwa nchi ilizingirwa katika shambulizi la kuvizia la wanajeshi wa kambi hii na kuangamizwa kikamilifu hapo jana.

Katika mapigano hayo, idadi ya wanachama wa timu ya magaidi waliuawa na kujeruhiwa, na vifaa vyao vilichukuliwa na wapiganaji wa Kiiislamu.Kituo cha Hamza Sayyid al-Shuhada cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (SEPAH) kimewaonya vibaraka wa ustikbari kimataifa na kutangaza kuwa, walinzi na wapiganaji shupavu wa kituo hicho wako macho na wanafuatilia kwa makini nyendo za maadui na kwamba, hatua ndogo kabisa dhidi ya usalama na umoja wa ardhi yote ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itakabiliwa na majibu makali na ya kumfanya adui ajute kwa chokochoko yake.


342/