Main Title

source : Parstoday
Jumatano

10 Julai 2024

15:12:08
1471076

Mkuu wa IRGC asema Jamhuri ya Kiislamu imelemaza nguvu ya Marekani

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema katika miongo kadhaa iliyopita Iran imemomonyoa uwezo wa Marekani na kuigeuza kuwa dola "dogo na dhaifu".

Akizungumza katika mji mtakatifu wa Mash'had huko kaskazini mashariki mwa Iran, Meja Jenerali Hossein Salami amesema kuwa hali ya Marekani hii leo hailinganishwi na hali yake miongo miwili au mitatu iliyopita.

Vilevile amezungumzia kutekwa ubalozi wa Marekani mjini Tehran, uliojulikana zaidi kama Pango la Ujasusi, kulikofanywa na kundi la wanafunzi wa Iran mnamo Novemba 1979, akisema ni jambo ambalo halikutasawarika.

"Tumefifiza nguvu ya Marekani. Marekani imekuwa ndogo na dhaifu, na taratibu imepoteza uwezo wake kwa sababu ya mmomonyoko uliosababishwa na Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran," amesema Kamanda Mkuu IRGC.

Salami pia amebainisha kuwa maadui wameshindwa kuitenga Iran kwa kuiwekea vikwazo vya kiuchumi na kuiba meli zake za mafuta huku Iran ikichukua hatua za kulipiza kisasi.

“Walikamata meli zetu huko Gibraltar; nasi tulitwaa meli zao katika maji ya Ghuba ya Uajemi na kuwafanya wajutie walichokifanya,” amesema Meja Jenerali Hossein Salami. Ameongeza kuwa Jamhuri ya Kiislamu imethibitisha kuwa "dunia ni kubwa zaidi kuliko Marekani na kwamba Marekani ni ndogo zaidi kuliko dunia."

342/