Main Title

source : Parstoday
Jumatano

10 Julai 2024

15:13:54
1471077

UN: Theluthi moja ya shule za UNRWA huko Gaza zimeshambuliwa na Israel, zimekuwa maeneo ya vifo

Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA), Philippe Lazzarini, amesema leo Jumatano, kwamba shule za Ukanda wa Gaza zimegeuka kuwa sehemu za taabu na vifo.

Razzarini ameongeza kuwa, shule nne za Gaza zimeshambuliwa kwa mabomu ya Israel katika muda wa siku nne zilizopita, na kwamba kwa ujumla thuluthi moja ya shule za UNRWA zimeshambuliwa kwa mabomu tangu kuanza kwa vita vya Israel dhidi ya watu wa ukanda huo.

Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) ameongeza kuwa, Gaza si mahali salama tena kwa watoto, akisisitiza kuwa kupuuzwa waziwazi sheria za kimataifa za kibinadamu hakupaswi kuruhusiwa kuwa hali mpya ya kawaida.

Afisa huyo wa ngazi za juu wa Umioja wa Mataifa ameongeza kuwa, shule ambazo zilikuwa sehemu salama za elimu na matumaini kwa watoto zimegeuka kuwa kambi za wakimbizi zenye idadi kubwa ya watu, na wakati mwingine, maeneo ya vifo na tabu.Matamshi haya ya Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) yanakuja baada ya shambulio la anga la utawala katili wa Israel kuua makumi ya raia na kujeruhia wengine zaidi ya 53 katika shule inayohifadhi wakimbizi kwenye mji wa Abasan, mashariki mwa Khan Yunis. 

Majuzi pia jarida mashuhuri la masuala ya tiba na afya la The Lancet la Uingereza liliripoti kuwa, yumkini idadi halisi ya Wapalestina waliouawa shahidi katika mashambulizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gaza inazidi watu 186,000.


342/