Main Title

source : Parstoday
Jumatano

10 Julai 2024

15:14:39
1471078

Kuendelea mvutano kati ya Waziri Mkuu na Jeshi la Kizayuni

Mzozo kati ya Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu, na jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel unaendelea kuongezeka huko Tel Aviv.

Mvutano kati ya Netanyahu, na maafisa wa jeshi la utawala huo hauhusiani tu na siku za hivi karibuni, bali umekuwa ukiongezela tangu kuanza mauaji ya kimbari huko Ukanda wa Gaza.

Kwa hakika mvutano huo umeongezeka katika siku za karibuni kutokana na kurefushwa vita vya Gaza na hasa kufuatia kuongezela hasira ya kimataifa dhidi ya utawala wa Kizayuni kutokana na jinai zake za kutisha dhidi ya watu wa ukanda huo.Baada ya kupita miezi tisa tangu utawala wa Kizayuni uvamie Ukanda wa Gaza bila ya kupata mafanikio yoyote muhimu, utawala huo unazidi kuzama katika migogoro ya ndani na nje siku baada ya siku. Hata baada ya muda huo, utawala wa Kizayuni haujafikia malengo uliyojiwekea wenyewe ya kuiangamiza Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (Hamas) na kuwakomboa mateka wa Kizayuni kutoka Ukanda wa Gaza.

Katika kipindi hiki, utawala wa Kizayuni haujapata mafanikio yoyote isipokuwa kufanya mauaji ya umati, uharibifu wa miundomsingi, jinai za kivita, ukiukaji wa sheria za kimataifa, ulipuaji wa mashirika ya misaada ya kibinadamu na kuwaweka njaa wakazi wa ukanda huo.

Jambo jingine ambalo limeibua mvutano kati ya pande hizo ni mazungumzo na harakati ya Hamas. Mazungumzo ya kuhitimisha mashambulizi ya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza yalianza Ijumaa huko Doha, mji mkuu wa Qatar, mazungumzo ambayo yanaendelea huku kukiwa na tofauti kubwa kati ya jeshi na Benjamin Netanyahu. Al Jazeera iliandika mapema kuwa tofauti za jeshi hilo katili na Netanyahu ziliongezeka baada ya taarifa ya msemaji wa jeshi, Daniel Hagari, kusema kwamba madai ya kuiangamiza Hamas ni hadaa tupu inayolenga kupotosha fikra za waliowengi duniani.

Hagari alisisitiza kuwa iwapo baraza la mawaziri la Kizayuni halitapata mbadala wa harakati hiyo, Hamas itaendelea kuwepo kwa sababu ni itikadi, na kuwa yeyote anayedhani kuwa Israel inaweza kutokomeza harakati hiyo anakosea sana.

Matamshi ya Daniel Hagari, kuwa Hamas itaendelea kubakia katika Ukanda wa Gaza hata kwa muda wa miaka 5 baada ya kumalizika vita, yamemkasirisha sana Benjamin Netanyahu. Kanali ya 14 ya utawala wa Kizayuni imeripoti kuwa, Netanyahu alikosoa vikali matamshi hayo ya Hagari katika kikao cha faragha cha Baraza la Mawaziri la Vita huko Tel Aviv.Kabla ya hapo mvutano ulikuwa umeibuka kati ya Netanyahu na Yuav Gallant, Waziri wa Vita wa Israel, katika mkutano wa baraza la mawaziri. Kanali ya 12 ya Televisheni ya utawala wa Kizayuni iliashiria suala hilo na kusema kuwa katika kikao cha baraza la mawaziri ambacho kilihudhuriwa na Gallant, Netanyahu alimkosoa vikali waziri huyo na kumfokea kwa kumwambia: "Wewe si waziri mkuu hapa." Baada ya hapo, Gallant alitaka kufanya vikao tofauti na wakuu wa Shirika la Ujasusi wa Nje (Mossad) na Ujasusi wa Ndani (Shabak) ili kujadili makubaliano ya kuachiliwa mateka wa Israel, lakini Netanyahu akazuia kufanyika vikao hivyo. Yisrael Zif, jenerali mstaafu wa Kizayuni, alisema katika taarifa kwamba jeshi la utawala wa Israel limeharibu malengo yake ya vita huko Gaza. Vile vile katika mahojiano na jarida la Wall Street Journal, Jenerali huyo wa Kizayuni ameongeza kuwa mvutano kati ya jeshi na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu umefikia kiwango cha juu kabisa na kuwa unaendelea kuongezeka kila siku. Nukta nyingine muhimu ni kuwa, kuongezeka mvutano kati ya Netanyahu na maafisa wa kijeshi wa utawala wa Kizayuni kumepelekea wakosoaji na wapinzani wake kuibua tena suala la kufanyika uchaguzi wa mapema wa bunge na kuvunjwa baraza la mawaziri.

342/