Main Title

source : Parstoday
Jumatano

10 Julai 2024

15:16:09
1471079

Umoja wa Ulaya walaani jinai za Wazayuni Khan Yunis

Josep Borrell, Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya amelaani mauaji ya raia yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni huko Khan na kusema kuwa: Je, raia wasio na hatia watavumilia hadi lini mzozo huu mkali?

Borrell ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa X: Jeshi la Israel lilishambulia familia zilizopata hifadhi katika shule moja huko Khan Yunis, na kulingana na ripoti, makumi ya watu waliuawa. Je, raia wasio na hatia watastahimili moto wa vita hivi hadi lini? Tunalaani ukiukaji wowote wa sheria za kimataifa na wale waliohusika lazima wawajibike.

Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya amesisitiza kuwa, kuna ulazima wa kusitishwa kwa mapigano mara moja ili kuruhusu raia walionasa katika vita hivyo wapate fursa ya kupumua, kuachiliwa kwa mateka wote na utoaji wa misaada muhimu ya kibinadamu.Jana Jumanne, utawala wa Kizayuni ulifanya jinai nyingine kwa kuishambulia shule ya al-Awda katika mji wa Abasan, mashariki mwa Khan Yunis, kusini mwa Ukanda wa Gaza, na ripoti zinaonyesha kuwa watu wasiopungua 29 wameuawa shahidi katika shambulio hilo. Wakimbizi wa Kipalestina walikuwa wamepatiwa hifadhi katika shule hiyo. Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Ukanda wa Gaza, idadi ya Wapalestina waliouwa shahidi hadi hivi sasa tangu tarehe 7 Oktoba 2023 imepindukia watu 38,000 huku zaidi ya 87,000 wakijeruhiwa. Wanamuqawama wa Palestina wakiongozwa na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS wameendelea kukabiliana na jinai za kijeshi za utawala wa Kizayuni hususan katika mji wa Rafah wa kusini mwa Ukanda wa Gaza. 

342/