Main Title

source : Parstoday
Jumatano

10 Julai 2024

15:17:06
1471081

Shirika la Afya Duniani: Ukanda wote wa Gaza sio salama

Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) amesema kuwa, hali ya usafi ya Ukanda wa Gaza sio nzuri na hakuna mahali salama katika eneo hili.

Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ameongeza kuwa hospitali ya "Al-Mamadani" kwa sasa haifanyi kazi, na hospitali za "Kamal Al-Adwan" na "Indonesia" pia zinakabiliwa na uhaba mkubwa wa mafuta, vitanda na vifaa vya matibabu.

Mkuu wa Shirika la Afya Duniani ameeleza kuwa,  kwa sasa hakuna sehemu salama katika Ukanda wa Gaza, na amri ya kuhama eneo hilo inazuia utoaji wa huduma ya kuokoa maisha.Hayo yanajiri katika hali ambayo, maelfu ya majeruhi na wagonjwa katika Ukanda nwa Gaza pia wanahitaji kusafiri nje ya nchi ili kukamilisha michakato ya matibabu au kupata huduma za matibabu ambazo hazipo huko Gaza hata hivyo Israel inakwamisha suala hilo. Wakati huuo huo, shirika la haki za binadamu la Ulaya na Mediterania limetahadharisha kuwa majeruhi na wagonjwa wa Kipalestina zaidi ya elfu 26 wanakabiliwa na hatari ya kifo huko katika Ukanda wa Gaza kufuatia kuendelea mashambulizi ya jeshi la utawala haramu wa Israel dhidi ya eneo hilo.

342/