Main Title

source : ABNA
Alhamisi

11 Julai 2024

08:28:37
1471191

Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia: Tofauti za kimadhehebu kati ya Sunni na Shia hazina manufaa yoyote

Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia, Mahathir bin Mohammad, alisema: "Lau Waislamu wangelikuwa kambi moja, Wapalestina wa Gaza wasingekabiliwa na mauaji na dhuluma nyingi kiasi hiki".


Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - "Mahathir bin Mohammad", Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia, akiwa katika mkutano wa faragha uliofanyika nchini Uingereza na kuhudhuriwa na idadi ya viongozi na wanaharakati wa Kiislamu wa Uingereza, alisema yafuatayo:

"Lau Waislamu wangekuwa kambi moja, Wapalestina wa Gaza wasingelikabiliwa na mauaji na mateso haya yote".

Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia, aliendelea kubainisha kwamba kwa kuzingatia kwamba msaada wa Marekani na nchi za Magharibi kwa Israel ni kinyume na maadili yote ya Kidemokrasia na Haki za Binadamu ambazo wao wenyewe wamekuwa wakizinadi katika historia yao yote; hivyo akatoa wito kwa Ulimwengu huru kujitahidi kukomesha mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina huko Gaza.

Aidha; alisisitiza kuwa kimsingi Waislamu ni kundi moja, kwa sababu Qur'an yao ni moja na Mtume wao pia ni yule yule mmoja.

Katika mazungumzo marefu na ya wazi yaliyodumu kwa takriban saa mbili kati yake na viongozi wapatao 50 wa jumuiya za Waislamu wa Uingereza, Wanazuoni na Wafanyabiashara, Mahathir alisisitiza kwamba: Kuendelea kushadidisha tofauti za kimadhehebu na kidini kati ya Waislamu wa Kissuni na Kishia hakuna manufaa yoyote.