Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

12 Julai 2024

16:38:48
1471476

Khatibu wa Swala ya Ijumaa Tehran: Wairani wamezima njama za maadui kwa kushiriki kwa wingi kwenye uchaguzi wa rais

Imamu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema: "Watu wa Iran wamezima njama za maadui kwa kushiriki kwa wingi kwenye upigaji kura katika uchaguzi wa rais Ijumaa wiki iliyopita."

Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami khatibu wa Swala ya Ijumaa wiki hii mjini Tehran amemshukuru Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kutokana na usimamizi wake makini katika siku 50 za kipindi cha baada ya kufariki dunia rais Ebrahim Raisi na kuongeza kuwa, "waliyoyafanya wananchi wa Iran katika awamu hizi mbili za uchaguzi wa rais yanawashangaza walimwengu; Wairani wametumbukiza kura milioni 55 kwenye masanduku ya kupigia kura katika awamu mbili za uchaguzi wa rais." 

Imam wa Swala ya Ijumaa ya Tehran amesema: Adui alikuwa akifanya njama za kutaka wananchi wasusie uchaguzi na kuzusha hali ya kukata tamaa, lakini wananchi, ambao wamekuwa wapiganaji na Mujahidina katika njia ya Mwenyezi Mungu, wamezima njama za maadui kwa kushiriki kwa wingi katika zoezi hilo.Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami, amewausia Waislamu kumchamungu, akisema: Imam Hussein (as), ambaye tuko katika kumbukumbu ya kuuawa kwake shahidi, alitoa wito wa kumcha Mungu katika mapambano yake ya Siku ya Ashura. Amewasihi Waislamu kutanguliza mbele taqwa na uchamungu, kuchunga mipaka ya Allah na kutohadaiwa na dunia.

342/