Kwa mujibu wa shirika la habari la Fars, Mohammad Bagher Qalibaf, jana Alkhamisi alikutana na kuzungumza na Rais Vladmir Putin wa Russia pambezoni mwa mkutano wa kilele wa BRICS na kusisitiza kuwa, ukiritimba wa Marekani bila ya shaka yoyote nao utakoma.
Kwa upande wake Rais Vladimir Putin amesema kwenye mazungumzo hayo kwamba, Uchaguzi wa Rais uliofanyika hivi karibuni nchini Iran umenipa matumaini na imani kwamba, uhusiano kati ya Iran na Shirikisho la Russia utaendelea kwa kasi ile ile iliyokuwepo huko nyuma wakati wa hayati Rais Ebrahim Raisi.
Rais Putin pia amesema kuwa, Spika wa Bunge la Russia (Duma) ataongoza ujumbe wa nchi hiyo katika sherehe za kuapishwa Rais mpya wa Iran.
Vile vile ameongeza kuwa: Iran imekuwa mwanachama rasmi wa BRICS na tumefurahishwa sana na hili, tuliunga mkono uanachama wa Iran katika kundi la BRICS.
Ikumbukwe kuwa Spika wa Majilisi ya Ushauri wa Kiislamu yaani Bunge la Iran alielekea nchini Russia siku ya Jumatano kwa lengo la kushiriki katika Kikao cha 10 cha Mabunge ya nchi wanachama wa kundi la BRICS.
342/