Main Title

source : Abna
Ijumaa

12 Julai 2024

21:28:36
1471553

Ayatullah Ramadhani:

"Maqam Mahmoud" (Daraja ya Kusifika) ndio lengo la juu katika Ziarat ya A'shura / Imam Hussein (a.s); ni mfano hai wa kujitolea zaidi wa ubinadamu

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s) amesema akibainisha kwamba: “Maqam Mahmoud” ni lengo la juu katika Ziarat ya A'shura, ambapo alieleza sifa za nafasi hii na akatolea mfano wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w).

 Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Ayatullah "Ridha Ramadhani" katika moja ya mikusanyiko ya Majalisi za Maombolezo ya Imam Hussein(a.s), alibainisha kuwa: Ziarat ya A'shura ni moja ya dua ambazo ni lazima maandalizi (utangulizi wake) yake yatimizwe; alibainisha akisema: Maneno yanayotamkwa katika ndimi zetu katika Ziarat hii, ni lazima tuyazingatie sana.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt(a.s) amesema kuwa: Haitoshi kwetu sisi kusoma (kutamka) maneno katika Dua; bali ni lazima tutambue (na kutimiza) maana ya maneno hayo; aliongeza akisema kuwa: Kama tunavyoomba (Allah) katika dua tukisema: Kila masikini mfanye kuwa tajiri; na mfunike (mvishe) kila mtu aliyeuchi (asiyekuwa na vazi); basi ni lazima tujitahidi kufanya utangulizi / maandalizi ya hilo tunaloliomba.

Aliongeza kusema: Katika Ziarat ya A'shura, tunamuomba Mwenyezi Mungu atufikishe kwenye utukufu kupitia elimu na maarifa ya Ahlul-Bayt (a.s). Vile vile tunamuomba Mwenyezi Mungu atujaalie siku tuwe ni wenye kujitenga na maadui wa Ahlul-Bayt (a.s), yaani: Maadui wa uadilifu, na maadui wa mambo ya kiroho na ubinadamu.

*Ukosefu wa maadili na uaminifu katika (serikali au) mifumo ya (Utawala ya) kimagharibi

Ayatullah Ramadhan ameashiria kuwa, muunganiko wa uaminifu na siasa hauna maana yoyote katika mfumo wa kimagharibi, na akasema: Pia katika mfumo wa kimagharibi hakuna mtazamo wa Kiakhera kuhusu uadilifu na heshima. Maadili na siasa havina maana katika mfumo wa kimagharibi

Akiashiria kwamba "hatua ya ukweli" (Qadam Sidiq) kuwa inapata maana katika elimu (maarifa) ya ufunuo; aliongeza kwa kusema: "Mtazamo wa Magharibi wa juu ya utu na haki (uadilifu) ni mtazamo wa juu juu wa ustawi wa kisekula." Katika mifumo ya Magharibi, dini haina nafasi hata kidogo

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya (a.s) alisema: Kwa kuisoma Ziarat ya A'shura, tunapata uchambuzi sahihi wa sisi wenyewe na jamii yetu, mtu anayesoma Ziarat ya A'shura anapata kuwa na madai makubwa kwamba lazima awe na dalili kwa ajili yao (hao watu wa jamii yake).

Amefahamisha na kubainisha zaidi kuwa: Leo hii, vitabu vingi vimeandikwa katika nchi za Magharibi katika kutetea haki za wanyama, lakini kwa upande mwingine, viko kimya kuhusu watoto na wanawake waliouawa Shahidi huko Gaza.

*Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w); Ni kielelezo cha maarifa, kiroho na haki (uadilifu)

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s) aliendelea kuashiria na kutilia mkazo ibara hii akisema: “Na anithabitishe kwenu kwa hatua ya ukweli katika dunia na Akhera” na akaashiria na kusistiza: Ili kuifikia hatua ya ukweli; ni lazima tuchukue hatua mbili: Kwanza: Tubadili mtazamo wetu; kisha kwa kuzingatia mtazamo huu tuchukue hatua (stahiki na sahihi).

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake amesema (akinukuu kipande cha Ziarat ya A'shura): “Na ninamuomba anifikishe kwenye (daraja) cheo cha kusifika kwenu mbele ya Mwenyezi Mungu, na aniruzuku kulipa nikiwa na pamoja na Imam wa Uogofu anayesema ukweli akitokana nanyi; na ninamuomba Mwenyezi Mungu kwa haki yenu."

Ayatullah Ramadhani; akiashiria kuhusu: "Daraja ya Kusifika" kuwa ni nafasi ambayo Mwenyezi Mungu amempa Mtume wake (s.a.w.w); ambapo maana yake (mafuhumu yake) ni "Uombezi" na "Kumshika (mja) mkono duniani na akhera"; aliongeza kwa kusema kuwa: Mtukufu Mtume (s.a.w.w) ni kiigizo cha kuigwa katika "Elimu / Sayansi", "Masuala ya kiroho" na "Haki".

*Imam Hussein (a.s); ni mfano bora wa kujitolea zaidi wa ubinadamu

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s) alisema kwamba: Wa pekee anayepaswa kushukuriwa ni Mwenyezi Mungu, lakini wale ambao wamefungamana na Mtukufu Mtume (s.a.w.w) pia wana sifa ya kusifika; akasema: Tabia ya Mtume (s.a.w.w) ilikuwa ni kiigizo chema, na shukrani, na kuleta Sasa alama na amani. "Daraja ya Kusifika" maana yake ni: Cheo / Nafasi ambayo mtu anaifikia na kustahili kusifiwa na kushukuriwa.

Ayatullah Ramadhani aliashiria tukio la A'shura na utengenezaji mkubwa wa Hamasa wa Aba Abdillah al-Hussein (a.s); ambapo alisema:

Imam Husein (a.s) alijitolea kila kitu chake (Fisabilillah), ikiwa ni pamoja na familia yake na watoto wake, (yote hayo) kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (s.w.t).