Shirika la habari la Mehr limenukuu ripoti za vyombo vya habari vya Saudia vilivyosema kuwa, Rais mteule wa Iran na Mrithi wa Ufalme wa Saudi Arabia wamesisitiza kustawishwa uhusiano wa pande mbili katika mazungumzo waliyofanya kwa njia ya simu.
Bin Salman amesema katika mazungumzo hayo ya simu kuwa, anaridhishwa na mwenendo wa kuimarika zaidi uhusiano wa Saudia na Iran katika nyuga tofauti, akisisitizia haja ya kupanuliwa zaidi ushirikiano huo wa pande mbili.
Dakta Pezeshkian kwa upande wake amesisitiza kuwa, kipaumbele cha sera za kigeni za Iran ni kupanua ushirikiano na majirani zake, na uhusiano huo uwe umejengeka katika msingi wa kuheshimiana pande mbili.
Jamhuri ya Kiislamu na Saudi Arabia hivi sasa zimo kwenye mkondo wa kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa kiuchumi na kidiplomasia wa mataifa haya mawili.
Daktari Masoud Pezeshkian, alichaguliwa kuwa rais mpya wa Iran kwa kura nyingi za wananchi katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais iliyofanyika Julai 5, mwaka huu 2024.
342/