Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

18 Julai 2024

16:07:09
1472882

Wabunge kukutana na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu siku ya Jumapili

Msemaji wa Bodi ya Uongozi ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amesema kuwa, wabunge wa bunge jipya watakutana na Ayatullah Khamenei, Kiongozi Maudhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu siku ya Jumapili.

Akizungumza na vyombo vya habari vya Iran, Alireza Salimi, Msemaji wa Bodi Inayosimamia Shughuli za Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema leo Alhamisi kwamba kikao cha bunge kimepangwa kumalizika mapema kuliko wakati wa kawaida Julai 21 ili kuwapa wabunge fursa ya kwenda kuonana na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei.

Bunge jipya la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran lilianza kazi Mei 27, mwaka huu, miezi michache baada ya wabunge hao kuchaguliwa katika uchaguzi wa bunge wa Machi 1, uliofanyika katika pembe zote za nchi.

Mkutano huo wa tarehe 21 Julai, siku ya Jumapili utakuwa wa kwanza rasmi kufanyika kati ya wabunge hao wapya na  Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

342/