Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

20 Julai 2024

15:50:03
1473265

Utayari wa Iran wa kushirikiana katika kuimarisha amani na usalama katika eneo

Amir Saeid Iravani Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, Iran iko tayari kushirikiana na nchi nyingine katika fremu ya Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai na Umoja wa Mataifa ili kukabiliana na changamoto za dharura na kuimarisha amani na usalama katika eneo.

Amir Saeed Iravani, amesema katika kikao cha Baraza la Usalama la umoja huo kwamba kwa kuzingatia changamoto za Afghanistan, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaamini kuwa ushirikiano kati ya taasisi hizo unaweza kuimarisha pakubwa utulivu na kuleta maendeleo katika nchi hiyo.
Amir Saeid Iravani ameongeza kuwa katika mazingira magumu ya hivi sasa kimataifa, kudumishwa amani na usalama wa kimataifa kunahitajia ushirikiano katika ngazi ya kitaifa, kikanda na kimataifa, na kuwa kuimarishwa ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na taasisi za kieneo ni muhimu sana sasa kuliko wakati mwingine wowote. Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema, kwa kulielewa vizuri suala hili, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inathamini majukumu ya Jumuiya ya Makubaliano ya Pamoja ya Usalama, Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai na Jumuiya ya Nchi Huru za Maslahi ya Pamoja katika kuimarisha amani na utulivu duniani. Amesema mapambano dhidi ya ulanguzi wa dawa za kulevya na aina nyingine za uhalifu uliopangwa kimataifa ni changamoto inayozitatiza nchi zote, ambayo inaweza pia kutoa fursa za maingiliano ya kivitendo kati ya Umoja wa Mataifa na Shirika la Ushirikiano la Shanghai.
 Saeid Iravani amesema mwishoni mwa hotuba yake kwamba Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai kwa kuzingatia muundo wake wa pande kadhaa, inaweza kuchangia pakubwa katika juhudi za kimataifa za kupambana na ugaidi na misimamo mikali ya kupindukia mipaka.

342/