Akiwa bungeni, Masoud Pezeshkian amewashukuru wabunge wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu na akatoa wito wa kushirikiana nao ili kutatua matatizo ya nchi. Amesema na hapa ninamnukuu: "Nimesema katika mijadala na midahalo ya karibuni na sasa bungeni kwamba nchi haiwezi kuendeshwa kwa kuwepo hitilafu na mizozo; tunapasa kushikamana ili kutatua matatizo yanayotukabili kupitia uratibu, maelewano na ushirikiano."
Rais mteule wa Iran pia amezungumzia kuhusu uchaguzi wa rais wa karibuni hapa nchini kwamba wananchi wa Iran walijitokeza na kupiga kura licha ya propaganda zilizoendeshwa ili kususua uchaguzi na kuwazaba mdomoni kofi kali wapinzani ambao walikuwa wameketi ndani na nje wakiendesha propaganda na kuwachochea wananchi wasusie uchaguzi.
Muhammad Baqer Qalibaf Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu pia kabla ya hotuba ya Rais mteule; alimshukuru kwa hatua yake ya kwenda bungeni na akasema anataraji ataweza kufanya kazi kwa kufuata sheria na kanuni nyingine kwa umakini wa hali ya juu na vile vile kupita vikao kama hivyo kati ya serikali na bunge.
Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amesema mbele ya Pezeshkian kuwa: 'Uchaguzi wa rais ambao ulifanyika katika kipindi kifupi umeonyesha wazi kuwa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran una imani kubwa juu ya ushiriki wa wananchi.'
Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Qalibaf ameashiria jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza na ksuema: 'Utawala huo hivi karibuni umeshadidisha mshambulizi dhidi ya raia, shule na miundombinu katika eneo hilo, na sasa unakabiliwa na matatizo makubwa.'
342/