Main Title

source : Parstoday
Jumanne

23 Julai 2024

19:23:32
1474078

Iran: Kusimama imara watu wa Yemen ni fakhari kwa Umma wa Kiislamu

Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, kusimama imara uongozi, wapiganaji wanajihadi na wananchi wanamuqawama wa Yemen na kuwa bega kwa bega na watu madhulumu wa Palestina katika kukabiliana na utawala wa Kizayuni ni hatua ya kihistoria na ya kujivunia kwa Umma wa Kiislamu.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB, Ali Bagheri Kani ameyasema hayo katika mazungumzo aliyofanya kwa njia ya simu na Muhammad Abdussalam, msemaji na mkuu wa timu ya mazungumzo ya Serikali ya Uokovu wa Kitaifa ya Yemen, ambapo mbali na kulaani shambulio la hivi karibuni la utawala wa Kizayuni lililolenga vituo vya kiraia vya bandari ya Hudaidah ya Yemen ametilia mkazo pia mshikamano wa Iran na wananchi na Muqawama wa Yemen katika kukabiliana na jinai za utawala bandia wa Israel. Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran vilevile ameuelezea Muqawama wa kupigiwa mfano wa watu wa Ghaza, ubunifu wa uongozi na wananchi wanamuqawama wa Yemen wa kuwa bega kwa bega na kuwaunga mkono Wapalestina dhidi ya jinai za Wazayuni, pamoja na Operesheni ya Ahadi ya Kweli iliyotekelezwa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa ni matukio matatu yenye taathira kubwa ambayo yamejiri katika kipindi cha zaidi ya miezi tisa iliyopita na kupelekea kushindwa kimkakati kwa Wazayuni

Katika mazungumzo hayo, Muhammad Abdussalam, msemaji na mkuu wa timu ya mazungumzo ya Serikali ya Uokovu wa Kitaifa ya Yemen ameishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa ujumbe wake wa kutangaza mshikamano na wananchi na Muqawama wa Yemen dhidi ya hujuma za hivi karibuni za utawala wa Kizayuni katika ardhi ya Yemen na kulengwa vituo vya kiraia na utawala huo, kulikopelekea kuuawa shahidi na kujeruhiwa raia kadhaa na kuielezea hujuma hiyo kuwa ni dalili ya kuemewa na kushindwa vibaya Wazayuni.

 Msemaji wa Serikali ya Uokovu wa Kitaifa ya Yemen amelitaja suala la Palestina kuwa ni kadhia inayouhusu umma wote wa Kiislamu na akapongeza na kuenzi kusimama imara kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuwa bega kwa bega na wananchi wanamuqawama wa Palestina na msukumo wake wa kisiasa na uungaji mkno wake wa kiroho kwa Yemen katika nyuga mbalimbali yakiwemo mapambano ya pamoja dhidi ya Wazayuni.../

342/