Akizungumzia suala la kujiondoa Rais wa Marekani, Joe Biden katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa rais baada ya kubainika kuwa hana uwezo wa kiakili wa kuongoza nchi, Nasser Kan'ani amesema: "Kuja na kuondoka watu na serikali tofauti huko Marekani sio muhimu kwetu; jambo muhimu ni kwamba wamekuwa na siasa za uhasama dhidi ya Iran kwa miongo kadhaa, na kinachoweza kubadilisha anga ya uhusiano ni mabadiliko ya sera na mtazamo wa Marekani kuhusiana na Iran."
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameongeza kuwa: "Lililo muhimu kwa Iran ni kuwajibika Marekani na kurejea katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA. Iran iliheshima majukumu yake yote kwa mujibu wa mapatano hayo, na pande nyingine zinalazimika kutekeleza wajibu wao."
Makubaliano ya nyuklia yanayojulikana kwa kifupi kama JCPOA yalifikiwa tarehe 14 Julai 2015 kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kundi la 5+1 (Russia, China, Marekani, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani na ushiriki wa mwakilishi wa Umoja wa Ulaya katika Sera ya Kigeni na Masuala ya Usalama, na wiki moja baadaye yaliidhinishwa kwa Azimio 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Hata hivyo tarehe 8 Mei, 2018, rais wa wakati huo wa Marekani, Donald Trump, aliiondoa nchi yake katika makubaliano haya ya kimataifa na kurejesha vikwazo visivyo halali dhidi ya Iran.Katika upande mwingine, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa: Inasikitisha kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel unaendelea kufanya jinai huko Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kwa msaada wa Marekani na baadhi ya serikali za nchi za Magharibi.
342/