Mojtaba Yousefi ameashiria kufanyika bungeni sherehe za kuapishwa Rais mpya na kusema: Hadi sasa nchi 60 zimetangaza kuwa zitashiriki katika hafla hiyo. Amesema Marais wanne wa nchi, Maspika 12 wa mabunge na Mawaziri Wakuu 7 watahudhuria sherehe za kuapishwa rais mpya wa Iran.
Yousefi ameongeza kuwa: Makamu wa Rais watatu, Manaibu Waziri Mkuu wawili, Mawaziri wa Mambo ya Nje 14 na wageni wengine watashiriki katika sherehe za kuapishwa Rais mpya wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu atamuidhinisha Rais Mpya Masoud Pezeshkian tarehe 28 mwezi huu wa Julai katika hafla itakayohudhuriwa na maafisa wa kitaifa na kijeshi katika Husseiniya ya Imam Khomeini (MA) Kisha sherehe za kula kiapo zitafanyika Jumanne tarehe 30 mwezi huu wa Julai katika ukumbi wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu saa kumi alasiri kwa wakati wa hapa Tehran kwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na wageni waalikwa kutoka nje ya nchi. Dakta Pezeshkian mwenye umri wa miaka 69, alichaguliwa kuwa Rais wa tisa wa Iran baada ya kuibuka na ushindi wa kura milioni 16 na 384,403 kati ya zaidi ya kura milioni 30 zilizopigwa katika duru ya pili ya uchaguzi wa 14 wa Rais wa Iran Ijumaa iliyopita ya Julai 5. Mpinzani wake Saeed Jalili alipata kura 13,538,179.
source : Parstoday
Jumatano
24 Julai 2024
19:13:19
1474300
Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya sherehe za kumuapisha Rais ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran ametangaza kuwa nchi 60 duniani zimetangaza kuwa zitashiriki katika sherehe za kuapishwa Rais wa Iran wa serikali ya awamu ya 14.