Main Title

source : Parstoday
Jumatano

24 Julai 2024

19:13:43
1474301

Iran yakanusha tuhuma chapwa za Marekani, Uingereza na Ufaransa

Balozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa amemwandikia barua Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Umoja wa Matiafa na kukanusha tuhuma za uongo zilizotolewa na Marekani, Uingereza na Ufaransa dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu na kusisitiza kuwa tuhuma hizo zinatokana na chuki za madola hayo kwa taifa la Iran ya Kiislamu.

Wawakilishi wa Marekani, Uingereza na Ufaransa wametumia kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kilichojadili hali ya eneo la Asia Magharibi na Yemen na kutoa tuhuma za uongo kwamba eti operesheni za kijeshi za Yemen zinafanywa kwa silaha za Iran huku madola hayo ya kibeberu yakifumbia macho kikamilifu uungaji mkono wao wa kila upande kwa jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel kwenye Ukanda wa Ghaza.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Iran Press, Amir Saeid Iravani, Balozi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa jana Jumanne alimwandikia barua Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kusema kuwa, wawakiishi wa Marekani, Uingereza na Ufaransa kwa mara nyingine wamelitumia vibaya jukwaa la Baraza la Usalama kutoa tuhuma zisizo na msingi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Katika kikao hicho, mwakilishi wa utawala dhalimu wa Israel, utawala ambao mikono ya viongozi wake imejaa damu za watu wasio na hatia wa Palestina, naye kama madola hayo ya kibeberu ya Magharibi, ametumia vibaya jukwaa la Baraza la Usalama kutoa tuhuma za uongo na taarifa zilizopotoshwa kuhusu Iran.

Mwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa ni aibu na inavunja moyo kuona wanachama watatu wa kudumu wa Baraza la Usalama yaani Marekani, Uingereza na Ufaransa walinyamazia kimya jinai na mashambulio ya utawala wa Kizayuni dhidi ya miundombinu ya wananchi wa Yemen, na wakati wananchi wa Yemen wanapojibu, madola hayo yanajipa uthubutu wa kueneza tuhuma za uongo dhidi ya Iran.

342/