Mkutano wa Pili wa Kikanda wa Kupambana na Madawa ya Kulevya wa nchi jirani na Iraq umehudhuriwa na mawaziri wa nchi wanachama na wakuu wa polisi wa kupambana na mihadarati, ambazo ni Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Saudi Arabia, Jordan, Kuwait, Uturuki, Misri, Syria na Lebanon huko Baghdad mji mkuu wa Iraq.
Shirika la habari la IRNA limeripoti kuwa, Ahmad Vahidi Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran amesema katika mahojiano na waandishi wa habari akidokeza yale yaliyozungumzwa katika kikao cha Mkutano wa Pili wa Kikanda wa wa Kupambana na Madawa ya Kulevya huko Baghdad kuwa: Washiriki wa mkutano huo wameeleza mitazamo na maoni yao ili kuzidisha ushirikiano na umoja zaidi. Amesema mwishoni mwa mkutano huo kumetolewa taarifa kuhusu hatua zilizopigwa na haja ya kushirikiana zaidi nchi jirani na Iraq ili kupambana kikamilifu na biashara ya madawa ya kulevya katika. Ahmad Vahidi Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran ameutaja mkutano huo kuwa ni ubunifu mzuri na athirifu uliofanywa na Baghdad na kuongeza kuwa: Waziri Mkuu wa Iraq pia amewasilisha maoni muhimu kuhusu ushirikiano wa kikanda kwa ajili ya kupambana na magendo ya madawa ya kulevya.
342/