Ali Bagheri Kani Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran sanjari na kumshukuru Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan kwa kushiriki katika sherehe ya kuapishwa rais mpya wa Iran mjini Tehran, amesema kuwepo kwake ni kielelezo cha azma na nia ya dhati ya viongozi wa ngazi za juu wa Sudan ya kuimarisha uhusiano kati ya nchi mbili za Kiislamu.
Vilevile ameeleza matumaini kuwa, kutashuhudiwa kufunguliwa upeo mpya katika uhusiano wa pande mbili na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika duru za kimataifa.
Ali Bagheri Kani ametoa wito wa kuimarishwa ushirikiano kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Sudan katika duru za kimataifa kuhusiana na masuala yanayozihusu nchi mbili hizo na ulimwengu wa Kiislamu, na kuanzishwa utaratibu wa kukabiliana na kulaani jinai za kivita na mauaji ya kimbari ya Wazayuni huko Gaza, na kutetea haki za watu wasio na ulinzi wa Palestina.Kwa upande wake, Hossein Awad, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Sudan amepongeza kufanyika kwa uchaguzi wa rais nchini Iran na kusema: kuchaguliwa rais mpya katika mazingira salama, yenye afya na ya kidemokrasia na kukabidhiana madaraka kwa amani nchini Iran ni fahari na heshima kwa watu wa Iran na dunia.
Akielezea kufurahishwa kwake na safari yake ya pili mjini Tehran katika kipindi cha miezi miwili iliyopita, Hossein Awad amesisitiza hamu kubwa ya maafisa wa ngazi za juu wa nchi yake ya kuimarishaji na kustawisha uhusiano na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kama nchi rafiki na muhimu.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan pia amewasilisha ripoti kuhusu matukio ya hivi karibuni ya ndani ya nchi yake na mchakato wa kurejesha utulivu na usalama nchini humo licha ya uingiliaji wa nchi za kigeni, na ameshukuru himaya ya kisiasa wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa serikali na watu wa Sudan.
Pia ametangaza utayarifu kamili wa nchi yake kwa ajili ya ushirikiano na wa karibu na Jamhuri ya Kiislamu katika duru za kimataifa.
342/