Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

1 Agosti 2024

19:30:24
1475999

Utawala wa Kizayuni usubiri jibu kali kwa kumwaga damu ya Shahidi Ismail Haniyeh

Katika tukio jipya la kuibua chokochoko katika eneo, utawala ghasibu wa Kizayuni kwa mara nyingine tena umefanya kitendo kingine cha ugaidi kwa uungwaji mkono wa Marekani, ambapo umemuua shahidi Ismail Haniyeh kiongozi wa kisiasa wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) mjini Tehran.

Idara ya Uhusiano wa Umma ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu imetangaza kuwa Shahidi Ismail Haniyeh na mmoja wa walinzi wake waliuawa shahidi siku ya Jumatano  baada ya kushambuliwa makazi yao hapa mjini Tehran, saa chache baada ya kuhudhuria hafla ya kuapishwa rais mpya wa Iran, Masoud Pezeshkian.

Uzoefu unaonyesha kwamba wakati wowote utawala wa Kizayuni unapojikuta kwenya hali ngumu kutokana na matatizo ya ndani yanayotokana na kuongezeka mashinikizo ya muqawama, hujaribu kupunguza matatizo hayo ya ndani kupitia ugaidi na kueneza migogoro yake nje ya ardhi unazozikalia kwa mabavu huko Palestina.Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni, ambaye hajaweza kufikia malengo yoyote aliyoyatangaza katika kipindi cha miezi 9 iliyopita, likiwemo la kuifuta kabisa Hamas huko Gaza, sasa yuko chini ya mashinikizo makali ya kumtaka akubali kusitisha mapigano. Anadhani kuwa vitendo vya woga kama vile vya kuwaua kigaidi viongozi wa muqawama vitamsaidia kuendelea kusalia madarakani na kudhoofisha msimamo wa Hamas katika mazungumzo ya usitishaji vita vinavyoendelea huko Ukanda wa Gaza.

Hii ni katika hali ambayo kitendo cha kigaidi cha karibuni cha utawala wa Kizayuni mjini Tehran, ambacho hakingeweza kutekelezwa bila ya ridhaa na uungaji mkono wa Marekani, bila shaka kitakuwa na matokeo na madhara makubwa kwa utawala huo wa kigaidi. Kama walivyosisitiza viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na makundi ya muqawama, kitendo hicho cha ugaidi kamwe hakitasimamisha mapambano dhidi ya Wazayuni, bali hata kitaimarisha zaidi irada ya mrengo wa muqawama katika njia ya kupigania uhuru na ukumbozi wa mataifa ya eneo.

Nukta nyingine muhimu ni kuwa Shahidi Ismail Haniyeh alifika mjini Tehran kama mgeni mwalikwa wa sherehe ya kuapishwa rasmi Masoud Pezeshkian, rais mpya wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, na aliuawa shahidi akiwa katika ardhi ya Iran jambo ambalo linakiuka wazi sheria za kimataifa.Kwa hivyo mbali na kuwa ni haki ya wazi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kujibu jinai hiyo, makundi ya muqawama katika eneo pia yanaweza kuongeza mashambulio yao dhidi ya maeneo na maslahi ya Wazayuni na Wamarekani katika eneo. Kwa msingi huo ni wazi kuwa ni Wazayunini na Wamarekani ndio watabeba dhima ya kuvurugika zaidi hali ya usalama katika eneo hilli.

Kuhusiana na hilo, Ayatullah Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, katika ujumbe wake wa rambi rambi kwa Umma wa Kiislamu, mrengo wa muqawama na taifa lenye fahari la Palestina kufuatia kuuawa shahidi Ismail Haniyeh, kiongozi shujaa, shupavu na mujahid wa Hamas, amesisitiza kuwa: "Kwa kitendo chake hiki, utawala wa Kizayuni unaotenda jinai na ugaidi umejiandalia mazingira ya kupewa adhabu kali, na ni wajibu wetu kulipiza kisasi cha damu ya shahidi Ismail Haniyeh iliyomwagwa kwenye ardhi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran."


342/