Kwa mujibu wa shirika la habari la ISNA, Nasser Kan'ani ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa X kwamba, kitendo cha utawala wa Kizayuni cha kumuua kigaidi kiongozi wa ngazi za juu wa kisiasa wa Palestina aliyekuwa ametembelea Tehran kushiriki katika sherehe za kuapishwa Rais wa 14 wa Iran, ni kitendo cha ugaidi wa kiserikali kilichopangwa kitaasisi na dola hilo dhalimu bila ya kujali kuwa kiongozi huyo wa HAMAS alikuwa mgeni rasmi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mwenye hadhi zote za kidiplomasia.
Mwanadiplomasia huyo wa ngazi za juu wa Iran vile vile amesema kuwa, ni jambo lisilo na chembe ya shaka kwamba, utawala wa Kizayuni ni tishio kubwa sana la amani na usalama wa dunia nzima ambao haujali wala kuheshimu sheria zozote za kimataifa.
Aidha amesema, kimya, kutojali na kutochukua hatua zozote nchi na taasisi za kimataifa mbele ya jinai kama hizo za kutisha, kunachochea vitendo zaidi vya ugaidi wa kiserikali na ni chokochoko hatari za Wazayuni dhidi ya usalama na amani ya mataifa ya dunia kama ambavyo pia ni kuhatarisha utulivu si wa ukanda huu tu, bali wa dunia nzima.
342/