Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

1 Agosti 2024

19:34:19
1476003

Kiongozi wa Mapinduzi kuongoza Sala ya Maiti ya kumsalia Shahidi Haniya, Iran yamuomboleza kwa siku tatu

Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu imetangaza kuwa, Ayatullah Khamenei leo asubuhi ataongoza Sala ya Maiti ya kumsalia Shahidi Ismail Haniya, Mwanjihadi mkubwa wa Muqawama wa Palestina, itakayosaliwa katika Chuo Kikuu cha Tehran.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Sala hiyo itasaliwa saa mbili na nusu asubuhi.

Wakati huohuo, Baraza la Uratibu wa Tablighi za Kiislamu limetangaza kuwa shughuli ya mazishi ya kuusindikiza na kuuaga mwili wa Shahidi Dkt. Ismail Haniya, Kiongozi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS, itaanzia katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Tehran baada ya kusaliwa na kuelekea eneo la Mzunguko wa Uhuru, Azadi.

Kufuatia kuuawa shahidi Kamanda Mwanajihadi Ismail Haniya, Serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza siku tatu za maombolezo nchini kote.Taarifa iliyotolewa na serikali imesema, kuuawa shahidi Ismail Haniya, Kamanda Mwanajihadi na Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS kumeutia majonzi Umma wa Kiislamu, wafuasi wa njia ya fikra ya Muqawama na watetezi wa ukombozi kote duniani na kuongeza kuwa, mauaji ya kiongozi huyo yameongeza ukurasa mwingine wa faili chafu na la kuaibisha la jinai zinazofanywa na tapo la kihalifu na ghasibu la Kizayuni.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa, Serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inalaani kitendo hicho cha kinyama kilichokiuka misingi na kanuni zote za kibinadamu na sheria za kimataifa kwa kumlenga mgeni rasmi na wa kidiplomasia wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliyekuja nchini kuhudhuria sherehe za kuapishwa rais, na inaitambua hatua hiyo kama alama nyingine ya wazi kabisa inayodhihirisha ugaidi wa utawala wa Kizayuni ambao kwa kuwepo kwake hakuna sehemu yoyote ya sayari hii ya dunia itakayosalimika na shari na uovu wa tezi hilo chafu. ../


342/