Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

1 Agosti 2024

19:35:31
1476005

Hizbollah yathibitisha kuuawa shahidi Fuad Shukr katika shambulio la anga la Israel

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon imethibitisha rasmi kuuawa shahidi Fuad Shukr mmoja wa makamanda wake wakuu katika shambulio la anga la Israel kwenye kitongoji kimoja jirani na mji mkuu Beirut.

Fuad Shukr, kamanda mwandamizi wa Hizbullah ya Lebanon, aliuawa shahidi juzi wakati ndege isiyo na rubani ya Israel iliporusha makombora matatu katika nyumba aliyokuwamo katika eneo moja karibu katika kitongoji cha Haret Hreik.

Duru za Lebanon zimeripoti kwamba, taarifa ya kuthibitishwa kuuawa kamanda huyo wa Hizbullah ilitangazwa jana na harakati hiyo ya muqawama.Katika taarifa hiyo, Hizbullah ya Lebanon imeashiria nafasi adhimu ya Fuad Shukr katika harakati za jihadi dhidi ya utawala haramu wa Kizayuni na kutetea kadhia ya Palestina na kueleza kuwa, hatua hiyo ya utawala ghasibu wa Israel ni jinai kubwa.

Shughuli ya kuuaga mwili wa kamnada huyo shupavu wa Hizbullah inafanyika leo katika viunga vya mji mkuu wa Lebanon Beirut ambapo Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Hizbullah anatarajiiwa kuhutubia.


342/