Mohammed Baqer Qalibaf, Spika wa Bunge la Iran amesema hayo leo mwanzoni mwa kikao cha hadhara cha Bunge na kusisitiza kwamba, sherehe za demokrasia ya kidini katika hhafla ya kuapishwa Rais wa Iran ziligeuka kuwa chungu kutokana na kuuawa shahidi hapa mjini Tehran Ismail Haniya Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Maambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS ambaye alikuwa mgeni wa Jamhuri ya Kiislamu.
Spika Qalibaf amebainisha kuwa, Iran itatoa jibu kali ambalo liitamfanya adyui na muungaji mkkono wakke yaani Marekani wajute na kutothubutu tena kufanya kosa la kijinga kama hilo.Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (SEPAH) jana lilitoa taarifa nambari tatu inayoeleza na kubainisha jinsi Ismail Haniya, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS alivyouawa hapa mjini Tehran.
Taarifa ya SEPAH ilieleza kuwa, jinai hiyo ya kigaidi iliyopelekea kuuawa shahidi Ismail Haniya ilipangwa na kutekelezwa na utawala haramu wa Israel kwa himaya na uungaji mkono wa serikali inayotenda jinai ya Marekani.
Sehemu nyingine ya taarifa hiyo ilibainisha kuwa, shambulio lililopelekea kufa shahidi Ismail Haniya lilitekelezwa kwa kifaa cha kupiga masafa mafupi kilichovikwa mada kali za milipuko chenye uzito wa karibu kilo saba. Shambulio hilo lilitekelezwa umbali wa masafa machache kutoka nje ya eneo la jengo alilokuwamo shahidi Ismail Haniya.
342/