Main Title

source : Parstoday
Jumanne

6 Agosti 2024

15:13:18
1477035

Pezeshkian: Iran iko tayari kuendeleza ushirikiano wa pande zote na Venezuela

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesiistiza kuwa Tehran iko tayari kupanua ushirikiano wa pande zote na Venezuela.

Rais Masoud Pezeshkian jana usiku alizungumza kwa simu na Rais Nicolas Maduro wa Venezuela na kumpongeza kwa kuendesha uchaguzi wa rais nchini humo ambapo Maduro ameibuka mshindi. Pezeshkian amelaani uingiliaji wowote wa kigeni katika masuala ya ndani ya Venezuela. Nicolas Maduro pia ameishukuru Iran kwa salamu za pongezi na kusisitiza kuwa Venezuela iko tayari na inataka kustawisha zaidi ushirikiano na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Rais Maduro amesema kuwa kuimarika ushirikiano kati ya pande mbili ni chanzo cha kupatikana maendeleo na ustawi wa nchi mbili.  

Uchaguzi wa Rais wa Venezuela ulifanyika Jumapili tarehe 28 mwezi uliopita wa Julai ambapo Nicolas Maduro ameibuka na ushindi kwa kupata asilimia 52 ya kura zilizopigwa. 

Serikali ya Marekani, kufuatia sera zake za kuingilia masuala ya nchi nyingine imehoji ushindi wa Maduro katika uchaguzi wa Venezuela na kudai kuwa, kwa mujibu wa ushahidi mwingi, mpinzani wake amepata kura nyingi zaidi katika uchaguzi wa rais wa mwezi uliopita. 


342/