Main Title

source : Parstoday
Jumapili

25 Agosti 2024

18:43:51
1480601

Sheikh Zakzaky: Utawala wa Kizayuni uko kwenye ncha ya kuporomoka

Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria amesema kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel unaelekea kudidimia kutokana na operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa.

Sheikh Ibrahim Zakzaky, ameyasema hayo katika maandamano ya Wito wa Al-Aqsa katika mji wa Karbala anakoshiriki kumbukumbu ya Siku ya Arubaini ya Imam Hussein (as) na kuongeza kuwa: Utawala ghasibu wa Israel umedhoofika na uko kwenye ncha ya kudidimia.

Sheikh Zakzaky amesema: Kuporomoka kwa utawala ghasibu kulianza kwa operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa, na kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu, utaangamia karibuni. Amesisitiza kuwa: "Hii sio kauli ya kutazamia ya kujipa matumaini, bali ushahidi uliopo unaonyesha hivyo."

Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria amesema: Leo na baada ya umwagaji damu mkubwa huko Gaza, kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu, Gaza itashinda, na baada ya hapo Palestina itashinda, na hivi karibuni tutatekeleza ibada ya Swala katika Msikiti wa Al-Aqswa. 

Vikiashiria mwenendo wa vita dhidi ya Ukanda wa Gaza na mauaji ya idadi kubwa ya wanajeshi wa Israel katika vita hivyo, vyombo vya habari vya utawala huo wa Kizayuni vimekiri kwamba, ahadi zilizotolewa na Waziri Mkuu, Benjamin Netanyahu, katika kipindi cha miezi 11 iliyopita kuhusu kushinda vita hivyo na kuiangamiza Hamas ni ndoto tupu na kauli za kuwahadaa watu. 

342/