Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

2 Septemba 2024

16:25:11
1482424

Araghchi asisitiza kuendelea sera za Iran za kuunga mkono muqawama

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza ulazima wa kuendelezwa sera za taifa hili za kuunga mkono Muqawama na mapambano dhidi ya utawala ghasibu wa Israel.

Sayyid Abbas Araghchi amesema hayo katika mazungumzo yake hapa mjini Tehran na Sayyid Abdallah Safieddin, mwakilishi wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon.

Wawili hao wamejadili matukio ya hivi karibuni katika eneo la Asia Magharibi na kuangazia pia hali ya hivi karibuni ya mapambano dhidi ya Israel huko Lebanon na matukio ya sasa katika Palestina, hususan Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza katika mazungumzo hayo juu ya kuendelea sera za taifa hili za kuunga mkono muqawama na mapambano dhidi ya utawala haramu wa Israel. Aidha ameongeza kuwa, sera za Iran za kuunga mkono muqawama na mapambano ni thabiti na kueleza kwamba, muqawama na mapambano ni haki halali ya mataifa ya eneo kwa ajili ya kukabiliana na uvamizi wa Wazayuni maghasibu.Katika upande mwingine, Abbas Araghchi Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameukosoa vikali utawala ghasibu wa Israel na kusema, ukatili wake usiokoma kuwa ndio sababu kuu ya kuongezeka hali ya wasiwasi na migogoro katika eneo la Asia Magharibi.

Amesisitiza haja ya kuchukuliwa hatua madhubuti na jumuiya ya kimataifa katika kukomesha mauaji hayo ya kimbari na kuwezesha kufikishwa misaada ya kibinadamu Gaza.


342/