Main Title

source : Parstoday
Jumanne

3 Septemba 2024

15:30:57
1482700

Jeshi la Iran lazindua Kifaru kipya cha teknolojia ya hali ya juu

Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limezindua kifaru kilichoboreshwa kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu ili kuimarisha uwezo wake wa kivita na kukabiliana na maadui.

Kifaru kilichoboreshwa cha M60 kilizinduliwa jeshini Jumapili katika hafla iliyohudhuriwa na Kamanda wa Kikosi cha Nchi Kavu cha Jeshi.

Jenerali huyo amesema kifaru cha M60 kina uwezo sawa na vifaru bora zaidi duniania kwani kina uwezo mkubwa  wa kivita. Aliongeza kuwa kifaru hicho "kimeboreshwa kulingana na teknolojia ya kisasa." 

Kamanda huyo alisema mchakato wa uboreshaji, umeimarisha vipengele vyote 13 vya mashine hiyo ya vita ikiwa ni pamoja na silaha tendaji, uendeshaji wa mchana na usiku, vifaa vya macho ambavyo vinawapa waendeshaji wake uwezo wa kuona maeneo yote ya medani ya kivita, mizinga yenye uwezo mkubwa, na injini ambazo zimeongeza kasi na uwezo wa kugeuka haraka.

Kifaru cha M60 sasa kitajulikana kama Soleimani-402, kumuenzi aliyekuwa kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Kiislamu, IRGC, Luteni Jenerali Qassem Soleimani aliyeuawa shahidi katika hujuma ya kigaidi ya Marekani mwaka 2020 akiwa nchini Iraq.

Heydari alisifu Kituo cha Uzalishaji, Uboreshaji na Ukarabati cha Shahidi Zarharan katika Wizara ya Ulinzi ambacho kimesimamia mchakato wa uboreshaji wa kifaru hicho.

Kwa kutii maagizo ya Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Iran, maafisa wa kijeshi nchini Iran wamesisitiza mara kwa mara kwamba nchi haitasita kuimarisha uwezo wake wa kijeshi, ambao unakusudiwa kikamilisha mchakato wa kujihami nchi, na kwamba suala hilo haliwezi kuwekwa katika meza ya mazungumzo.

Kwa kuegemea juhudi za wataalamu wa ndani ya nchi, Jamhuri ya Kiislamu imepiga hatua kubwa katika kuimarisha uwezo wa kujitosheleza wa vikosi vyake vya Jeshi, licha ya vikwazo vikali ilivyowekewa na Marekani na washirika wake.

342/