Main Title

source : Abna
Jumanne

3 Septemba 2024

19:51:03
1482773

Kujiuzulu kwa Kamanda wa Vikosi vya ardhini vya utawala wa Kizayuni

Gazeti la Times of Israel, likiwanukuu maafisa wa jeshi, lilitangaza kujiuzulu kwa kamanda wa vikosi vya ardhini vya Israel.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul_Bayt (a.s) - ABNA - Vyombo vya Habari vya Utawala wa Kizayuni viliripoti ongezeko la hitilafu baina ya taasisi mbalimbali za kijeshi na za kiraia za utawala wa Kizayuni kuhusiana na kubadilishana wafungwa na usimamizi wa vivuko vya mipakani.

Kwa mujibu wa Al Jazeera, gazeti la "The Times of Israel", likiwanukuu maafisa wa jeshi, lilitangaza kujiuzulu kwa kamanda wa vikosi vya ardhini vya Israel.

Wakati huo huo jeshi la Kizayuni limetangaza kuwa kamanda wa vikosi vya ardhini vya utawala huu amejiuzulu wadhifa wake kutokana na sababu za kibinafsi.

Kwa upande mwingine, wachambuzi wa mambo wanaamini kuwa, kujiuzulu huko kunatokana na kushadidi tofauti kuhusu kuendelea kwa vita vya Gaza, hasa baada ya miili ya mateka 6 kupatikana ndani ya handaki za Rafah.