Kwa mujibu wa duru hizo, Rexhepi alikuwa akisimamia shughuli za kifedha za Mossad nchini Uturuki, ambapo imefichuliwa kuwa, kwa maelekezo ya shirika hilo la ujasusi la Israel, jasusi huyo aliendesha operesheni za uchunguzi kwa kutumia ndege zisizo na rubani na operesheni za kisaikolojia dhidi ya wanasiasa wa Palestina. Rexhepi amegunduliwa kuwa alihamisha fedha kuwapatia maajenti wa ugani wa Mossad huko Uturuki ambao walikuwa wakikusanya taarifa za kijasusi kuhusu Syria.Taarifa zinaeleza kuwa, shughuli mbalimbali za Rexhepi, ikiwa ni pamoja na za uhamishaji fedha wenye kutia shaka kupitia akaunti zake, zilianza kufuatiliwa na MIT, ambapo uchunguzi ulibaini kuwa alihamisha kiasi kikubwa cha pesa kupitia wakala wa Western Union kuwapelekea maajenti wa ugani wa Mossad walioko Uturuki. Shughuli za jasusi huyo wa Mossad zilianza kufuatiliwa tangu alipoingia nchini Uturuki Agosti 25.
342/