Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

6 Septemba 2024

18:02:53
1483262

IRGC: Visiwa vya Iran katika Ghuba ya Uajemi vimetayarishwa kijeshi

Kamanda wa Kikosi cha Wanamaji katika Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amekagua utayarifu wa kijeshi katika eneo muhimu la kistratijia la Nazaat katika Ghuba ya Uajemi. Eneo hilo lina visiwa vinne vya Tunb Kubwa, Tunb Ndogo, Abu Musa, na Sirri karibu na Mlango-Bahari wa Hormuz.

Admeri Alireza Tangsiri alikagua ya vitengo vya IRGC vya majini na makombora katika eneo hilo siku ya Alhamisi.

Ofisi ya Habari ya IRGC imemnukulu akisema: "Kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu utayari wa kisaikolojia na kiutendaji wa wapiganaji wa Kiislamu uko katika kiwango cha juu".

Kamanda huyo alisisitiza umuhimu wa visiwa hivyo, akivielezea kama "eneo muhimu la operesheni" katika Eneo la Tano la Kikosi cha Wanamaji cha IRGC.

Amesisitiza kuhusu kutekeleza mwongozo wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyyed Ali Khamenei juu ya kudumisha hali ya juu ya utayarifu miongoni mwa vikosi vilivyoko hapo.

Admeri Tangsiri aliangazia nyongeza ya zana za kijeshi kwa kikosi hicho, akisema kuwa moja ya "lengo lake kuu" katika kuzuru visiwa hivyo lilikuwa kutathmini "ufanisi wa utendaji" wa mifumo ya ulinzi iliyosambazwa katika Visiwa na Mlango-Bahari wa Hormuz.

Amesema "mifumo yote, ikiwa ni pamoja na makombora, ndege zisizo na rubani, na vifaa vingine vya ulinzi, viko katika hali bora zaidi, vinafanya kazi kikamilifu kwa ajili kulinda amani na usalama wa taifa."

Akizuhutubu nchi jirani na washirika katika eneo la  Ghuba ya Uajemi na Bahari ya Oman, Admeri Tangsiri aliwasilisha ujumbe wa Jamhuri ya Kiislamu wa "urafiki, udugu na umoja," huku akilaani uwepo wa maadui wa kigeni katika eneo hilo kama chanzo cha "mgawanyiko na fitna. ”

Alisisitiza zaidi kwamba Jamhuri ya Kiislamu "itasimama imara" dhidi ya maadui wowote.

342/