Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

6 Septemba 2024

18:04:40
1483267

Hamas yapinga makubaliano yanayotambua rasmi uwepo wa Israel huko Ghaza

Mkuu wa timu ya mazungumzo ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, amesema harakati hiyo ya muqawama haitaafiki makubaliano ambayo yanahalalisha uwepo wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Ghaza.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IRIB, Khalil al-Hayya, mkuu wa timu ya mazungumzo ya Hamas amezungumza kuhusiana na usitishaji vita wa Ghaza na kusema: "Iwapo serikali ya Marekani inataka kufikia usitishaji vita na kufanikisha makubaliano ya kubadilishana mateka, ni lazima iache uungaji mkono usio na masharti kwa utawala wa Kizayuni wa Israel."

Al Hayya ameongeza kuwa: "Hatuhitaji mpango mpya, na pendekezo lolote kutoka upande wowote linapaswa kimsingi kumlazimu Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni kutekeleza yale yaliyokubaliwa hapo awali."

Mkutano mpya wa mazungumzo ya kumaliza vita Ghaza ulifanyika  Doha, Qatar kuanzia tarehe 15 hadi 16 Agosti. Kikao hicho ambacho pia kilijadili kubadilishana mateka kilihudhuriwa na wawakilishi wa Hamas, utawala wa Israel, Misri, Qatar na  Marekani.

Licha ya wito wa kimataifa wa kusitisha mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na utawala haramu wa Israel huko Gaza, mazungumzo kati ya Hamas na Israel hayajazaa matunda kutokana na ukaidi wa waziri mkuu wa utawala huo Benjamin Netanyahu na waitifaki wake wenye misimamo mikali.

Makundi ya wapigania ukombozi wa Palestina yamesema mazungumzo ya usitishaji yamefeli pia  kunatokana  kuendeleza mauaji ya kimbari na mauaji ya watu wasio na ulinzi yanayoendelezwa na utawala katili wa Israel huko Gaza.

342/