Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

6 Septemba 2024

18:06:27
1483271

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC atetea kibali cha kukamatwa Netanyahu

Mwendesha mashtaka mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu amesema kuwa, haki lazima itendeke baada ya kutolewa kibali cha kukamatwa kwa waziri mkuu wa Israel na waziri wa ulinzi wa utawala huo ghasibu.

Karim Khan amesema ni muhimu kuonyesha kwamba mahakama itashikilia mataifa yote kwa kiwango sawa kuhusiana na madai ya uhalifu wa kivita. Pia amefurahishwa na uamuzi wa serikali mpya ya Uingereza wa kuacha kupinga kutolewa kwa hati za kukamatwa Benjamiin Netanyahu.

"Kuna mabadiliko na ninafikiria ni ya muhimu kuhusiana na sheria ya kimataifa na serikali mpya. Na nadhani hilo linakaribishwaalisisitiza Karim Khan.

Mwezi uliopita, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) aliiwataka majaji wa mahakama hiyo watoe haraka waranti wa kukamatwa waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu na waziri wa vita wa utawala huo Yoav Gallant.Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC amesema, kuna sababu za kimantiki zinazothibitisha kuwa Netanyahu anahusika na jinai za kivita na jinai dhidi ya binadamu katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na akakumbusha kwamba, hakuna mpaka wa muhula uliowekwa kwa majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai wa kuamua kuhusu utoaji waranti wa kukamatwa viongozi hao wa utawala wa Kizayuni.

Tangu tarehe 7 Oktoba 2023, kwa uungaji mkono kamili wa Marekani na nchi za Magharibi, utawala ghasibu wa Kizayuni umekuwa ukifanya mauaji makubwa katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan dhidi ya wananchi wasio na ulinzi na madhulumu wa Palestina.


342/