Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio makamu wa Rais Rigathi Gachagua, alisema wanafunzi 70 hawajulikani walipo na 27 wako hospitali. Gachagua ameuitaja mkasa huo kuwa wa kutisha na kusema kwamba kazi ya uchunguzi kwa kutumia vinasaba DNA itahitajika ili kusaidia kuwabaini wahanga na kutoa wito kwa jamii kusaidia katika kuwatafuta waliopotea.Kenya: Wanafunzi 70 hawajulikani walipo kufuatia mkasa wa moto
Taharuki imetanda miongoni mwa familia za watoto zilizokusanyika shuleni hapo zikisubiri kupata taarifa. Kulingana na jeshi la polisi, miili ya watoto iliyopatikana katika eneo la ajali imeungua kiasi cha kutotambulika.
Jana Rais Willam Ruto wa Kenya alitoa amri ya kufanyika uchunguzi haraka iwezekanavyo kuhusiana na tukio la moto lililotokea katika Skuli ya Msingi ya Endrasha katika Kaunti ya Nyeri na kusababisha wanafunzi 17 kupoteza maisha na wengine 14 kujeruhiwa vibaya.
Msemaji wa kitengo cha Huduma ya Taifa ya Polisi, Daktari Resila Onyango amesema kuwa, timu ya maafisa wa uchunguzi imetumwa katika skuli hiyo iliyoko eneobunge la Kieni, Kaunti ya Nyeri.
342/