Vyombo hivi vya habari viliripoti kwamba rabi alimpongeza mmoja wa askari hawa.
Kulingana na video ya rabi huyu iliyochapishwa kwenye mitandao ya kijamii, anaonekana akimwambia askari huyo: "Wewe Utaachiliwa huru kabisa huna kosa". Kwani umefanya kosa gani? Wewe umempiga adui. Kila kitu kinakwenda vizuri. Lau ungekuwa mahali pengine, wangekupa tuzo!.
Mazouz ana asili ya Tunisia na ni miongoni mwa marabi wenye ushawishi mkubwa miongoni mwa Haredi (Mayahudi wenye misimamo mikali) na katika siasa za utawala wa Kizayuni, na watawala wa Israel wanatilia maanani maoni na maamuzi yake.
Mawaziri Wakuu na wanachama wa chama cha Likud wanashauriana na rabi huyu katika Baraza la Knesset (Bunge), na Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni, pia walikutana naye nyumbani kwake.
Kabla ya hapo Kanali ya 12 ya Televisheni ya utawala haram wa Kizayuni ilichapisha matukio ya kustaajabisha yanayoonyesha askari wa utawala huo ghasibu wakimbaka mfungwa wa Kipalestina katika jela ya Sedi Timan inayojulikana kwa jina la "Guantanamo ya Israel".
Hadi sasa kumekuwa na ripoti nyingi za hatua za kivamizi za utawala huo ghasibu dhidi ya wafungwa wa Kipalestina katika jela za utawala wa Kizayuni zikiwemo mateso makali, kunyimwa maji, chakula na huduma za matibabu.
Kwa mujibu wa Chama cha Wafungwa wa Kipalestina, utawala wa Kizayuni umewashikilia mamia ya Wapalestina kutoka Gaza tangu kuanza vita vya Gaza tarehe 7 Oktoba mwaka jana.