Kisha Salim Muhammad al-Doubi, mwenyekiti wa mashindano alihutubia hafla hiyo, akiangazia nafasi ya juu kabisa ya Qur’ani Tukufu na hadhi ya wahifadhi Qur'ani.
Al-Doubi pia ameyapongeza mashindano ya Sheikha Fatima Bint Mubarak akisema yamegeuka na kuwa tukio kubwa katika uwanja wa shughuli za Qur'ani kwa wanawake.
Jumla ya wahifadhi 60 wa Qur'ani kutoka nchi mbalimbali wanashiriki katika toleo hili la mashindano hayo.
Siku ya kwanza ilishuhudia washindani kutoka nchi 11, ambazo ni Myanmar, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Somalia, Ghana, Togo, Chad, Mali, Burkina Faso, Ufilipino, Eritrea na Rwanda.
Shindano hilo litaendelea hadi Septemba 13 katika Jumuiya ya Utamaduni na Kisayansi huko Dubai.
Tuzo la Kimataifa la Qur'ani Tukufu la Dubai (DIHQA) kila mwaka huandaa tukio la kimataifa la Qur'ani kwa wanawake kutoka nchi mbalimbali.
chanzo: IQNA