source : Abna
Jumatatu
9 Septemba 2024
18:59:34
1483994
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Kufuatia mashambulizi ya mara kwa mara ya wanajeshi wa Kizayuni katika maeneo mbalimbali ya Gaza, ni vigumu kupata maji safi ya kunywa katika Mji wa Khan Yunis, na Wapalestina wanaoishi katika eneo hili; wanalazimika kila siku kukaa kutumia masaa mengi katika foleni ili waweze kupata maji safi ya kunywa.