Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA- Kimefunguliwa kituo cha Dar Al-Qur'an "Hikmat" kutokana na mashauriano ya msimamizi wa masuala ya kitamaduni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Afrika Kusini; na wakati wa hafla iliyohudhuriwa na Ayatollah "Mahmoud Mohammadi Iraqi", Mjumbe wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul- Bayt (a.s) katika jiji la Pretoria» Mji Mkuu wa Afrika Kusini.
"Dar al-Qur'an" hii ni kituo rasmi cha kwanza cha elimu ya Qur'an cha Shia kufunguliwa nchini Afrika Kusini, na katika sherehe zake za ufunguzi, watu mashuhuri kama vile Ayatollah Mahmoud Mohammadi Iraqi, Ayatollah Ahmad Moballaghi, Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Dk. Ibrahim Buffalo, Sheikh Abdulaziz Sheikh na kundi la Wanazuoni wa Kiislamu kutoka Jumuiya mbalimbali za Shia na Sunni pamoja na shakhsia za Kikristo walikuwepo Afrika Kusini (katika sherehe hizo).