Alisema: Ikilinganishwa na Yazidiism (Uyazid), (Husseinism) Uhussein ndio roho ya kweli ya Uislamu, ambayo ni sauti ya haki na ukweli dhidi ya dhulma, ukandamizaji na batili ya kila zama.
Maqsood Ali Domki amesema: "Kuwaunga mkono Waislamu madhulumu wa Palestina dhidi ya dhalimu Israel ilikuwa ni moja ya matakwa ya Hussein (a.s), na kunyamazia dhulma na kunyamaza kimya mbele ya dhalimu ni jinai kubwa."
Katibu wa Baraza la Umoja wa Waislamu wa Pakistan alisema kwamba kwa tafsiri sahihi ya Uislamu, mtu anapaswa kuendelea na mwongozo wa Wilayat Faqih na mfumo wa kufuata marajii, na kuzingatia mkusanyiko wa mamilioni ya watu huko Karbala al_Mualla kama ishara ya hofu kwa ajili ya mayazidi wa Zama hizi za leo.
Alibainisha: Wafuasi wa Imam Hussein wa kila rangi na kila Taifa kutoka pande zote za Ulimwengu, walifika Karbala na kufanya upya Baia' yao kwa Imam wa Zama (a.t.f.s).