Main Title

source : Parstoday
Jumapili

15 Septemba 2024

19:56:15
1485511

Abdul-Malik al-Houthi: Marekani ni mshirika wa jinai za Israel huko Palestina

Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema kuwa, Marekani ni mshirika wa adui Mzayuni katika kuwaua watu wasio na hatia wa Palestina.

Sayyid Abdul Malik al-Houthi, Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen ameitaja misimamo ya Waislamu dhidi ya mauaji ya kimbari ya taifa la Palestina kuwa ni ya aibu na fedheha na kuongeza kuwa, adui mvamizi anaendelea kuwalenga wakimbizi wa Kipalestina katika mahema yao ya vitamba kwa kutumia mabomu angamizi ya Kimarekani na katika maeneo ambayo  yalitangazwa kuwa ni salama.

Al-Houthi ameeleza kuwa, baada ya miezi 11 ya utawala wa Kizayuni wa Israel kuuvamia Ukanda wa Gaza, hakuna harakati yoyote ya maana iliyochukuliwa iwe ni chini ya muuelekeo wa Uarabu na utaifa au chini ya mielekeo ya kisiasa, na hakuna chochote kilichowasukuma Waislamu kuchukua msimamo wa pamoja wenye maamuzi. 

Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen ameongeza kuwa, misimamo ya baadhi ya serikali, tawala na viongozi wa nchi za Kiarabu ni msimamo wa kushirikiana na adui  Israel na kushirikiana nao kulilenga taifa la Palestina.

Al-Houthi amesisitiza kuwa, Wamarekani ni washirika wa adui wa Israel katika matukio yote yanayotokea Palestina, na kuna mwelekeo wa pamoja wa Marekani na Israel. Marekani inachukua hatua za uadui, na kama si kufanyya hivyo, uhalifu wa Israeli haungetokea katika kiwango hiki, lakini bado Marekani inajionyesha kama mpatanishi.

342/