Main Title

source : Abna
Jumanne

17 Septemba 2024

07:12:52
1485833

Malaysia kuimarisha usaidizi kwa wahifadhi Qur'ani

Serikali ya Malaysia imethibitisha dhamira yake ya kuwawezesha vijana wanaohifadhi Qur'ani Tukufu ili kuhakikisha wanafaulu katika fani hiyo sambamba na kuwapa ujuzi katika nyanja zingine za kitaaluma.

Naibu Waziri Mkuu Ahmad Zahid Hamidi alitangaza uboreshaji wa Sera ya Kitaifa ya Elimu ya Tahfidh (DPTN).

Aidha waliohifadhi Qur'ani pia watawezesha katika sekta ya TVET (Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi) ili kuchanganya maarifa ya kidini na ujuzi wa kidunia," Zahid alisema katika chapisho kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook Jumapili.

Matamshi hayo yalifuatia Mkutano wa waliohifadhi Qur'ani katika Masjid Wilayah Persekutuan, uliosimamiwa na Waziri Mkuu wa Malaysia Anwar Ibrahim. Tukio hilo lilileta pamoja watu 24,000 walioihifadhi Qur'ani wakiwemo wanafunzi, walimu, na wanazuoni kutoka madrasah 1,500 za tahfidh ul Qur'an chini ya Taasisi ya Gabungan Persatuan Tahfidh ul Qur'an Kebangsaan (PINTA).

Zahid alisisitiza jukumu la mkutano huo katika kuonyesha juhudi za serikali za kuwawezesha wahifadhi Qur'ani kama viongozi wa baadaye katika masuala ya maadili na kiroho.

"Mwenyezi Mungu SWT aendelee kubariki juhudi hizi tukufu, na Qur'an iendelee kuwa nuru inayoongoza kila hatua tunayopiga kama Waislamu na watu wa Malaysia," alisema.

Ahmad Zahid alibainisha zaidi kuwa serikali inawatazama waliohifadhi Qur'ani Tukufu kama mtaji wa thamani wa binadamu na hivyo ni watu muhimu sana  kwa maendeleo ya taifa.

Alisisitiza umuhimu wa kuipa kipaumbele elimu ya Qur'ani huku akihimiza ukuaji wa kizazi kijacho katika majukumu ya kitaaluma na kijamii.

Malengo ya hafla hiyo ni pamoja na kuinua hadhi ya Qur'ani, kuhamasisha umoja, na kukipa uwezo kizazi cha vijana wanohifadhi Qur'ani ili waweza kuwa na nafasi muhimu katika mustakabali wa taifa.

IQNA