Aliyataja hayo katika Carnival (Sherehe) ya Mavazi ya Kidini na Mavazi ya Kienyeji iliyopewa jina la: "Kumfuata Mtume kwa ujumbe wa rehema kwa ajili ya Ulimwengu katika mfumo wa Uislamu" iliyofanyika katika eneo la "Siku bila Gari" kwenye Mtaa wa Jenerali Sudirman huko Jakarta, Indonesia.
Dkt. Omar Shahab aliendelea kusema: Natumai kwamba mpango huu utapanuliwa katika matukio mengine katika miaka ijayo na serikali ya mtaa wa Jakarta itauweka kama mpango wa kila mwaka wa kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Aliongeza: Kuna aina tofauti za uenezaji wa Kiislamu nchini Indonesia. Kwa maoni yangu, uenezaji wa Uislamu hauwezekani tu kupitia "Mihadhara na Elimu", lakini pia kupitia "Utamaduni", kwa sababu "Utamaduni" wa Indonesia ni "Utamaduni" wa Kiislamu.
Mkuu wa Jumuiya ya Wapenzi wa Mtume (s.a.w.w) alibainisha: Uislamu ni Dini ambayo ni rehema kwa Walimwengu wote na kwa namna fulani, ni Dini ya udugu.
Uislamu una sifa tatu za udugu, zikiwemo Udugu wa Kibinadamu (Udugu kati ya Wanadamu wote), Udugu wa Kiislamu (Udugu wa Kidini) na Udugu wa Kitaifa (Umoja katika mfumo wa Kitaifa).
Ikiwa sisi tutajitizama kama watu wa Indonesia, na kwa sababu ya umoja wetu na udugu wetu wa kitaifa; tunajiona kuwa sisi ni watu wa Taifa la Indonesia.
Sisi kama Wanadamu, tunaamini na kuitikadia ya kwamba Wanadamu wote wana Haki na wajibu sawa.
Pia, sisi kama Waislamu, tuna maadili yetu wenyewe ya Kiislamu.
Zaidi ya watu 500 kutoka rika tofauti kuanzia watoto, vijana hadi wazee walishiriki katika (carnival) sherehe hiyo ya Mavazi za Kidini na Mavazi za Kienyeji katika mnasaba wa kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Mtukufu Muhammad (s.a.w.w) katika Mji wa Jakarta.
Kipindi hiki kilivutia usikivu wa vyombo vya habari vya kitaifa vya Indonesia kama vile mtandao wa "TvOne" na Dazeni za vyombo vingine vya kuchapisha na kusambaza habari.