Main Title

source : Parstoday
Jumanne

17 Septemba 2024

16:54:11
1486048

HAMAS yapongeza shambulio la kombora la Yemen dhidi ya Israel

Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu wa Palestina HAMAS amepongeza na kusifu hatua ya jeshi la Yemen ya kushambulia eneo la jeshi la Israel huko Tel Aviv kwa kombora jipya la balistiki la hypersonic.

Yahya Sinwar, Mkuu mpya wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya HAMAS amesema hayo katika ujumbe aliomtumia Abdul-Malik al-Houthi, Kiongozi wa harakati ya Ansarullah nchini Yemen.

Sinwar amesema katika ujumbe huo kuwa: "Tunaishukuru Harakati ya Ansarullah ya Yemen kwa mapenzi yake ya dhati, azma na nia thabiti ya kupambana na dhulma na ukandamizaji wa Israel."

Kiongozi huyo mwandamizi wa HAMAS amebainisha kuwa, "Operesheni ya jeshi la Yemen kufika kwenye kina kirefu cha utawala wa Kizayuni na kupiga maeneo ya adui imeleta uhai mpya katika Operesheni ya Kimbunga cha al-Aqsa na kutoa pigo jipya kwa mradi wa utawala wa Tel Aviv katika eneo."

Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu wa Palestina HAMAS amebainisha kuwa, "Operesheni ya Yemeni ilituma ujumbe wa wazi kwa Israeli kwamba njama za kuzuia na kujitenga zimeshindwa na pande zinazounga mkono Palestina kutekeleza mbinu bora na yenye ushawishi zaidi,"

Msemaji wa jeshi la Yemen Brigedia Jenerali Yahya Saree amesisitiza kuwa kombora hilo jipya la balistiki la Hypersonic lilirushwa hadi Tel Aviv kwa kutumia muda wa dakika 11 na sekunde 30 katika umbali wa kilomita 2040; jambo lililowatia kiwewe na hofu Wazayuni na kupelekea Wazayuni zaidi ya milioni mbili kukimbilia mafichoni. 

Yahya Sinwar amelipongeza pia taifa zima la Yemen na kueleza kuwa, Wayemen wamekuwa waungaji mkono wakubwa wa Wapalestina na malengo yao halali katika kipindi chote cha historia.

342/