Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

20 Septemba 2024

20:14:07
1486842

Data za Waindonesia milioni sita akiwemo Rais na wanawe zavujishwa na kuuzwa tovutini

Data za walipakodi milioni sita katika taifa la nne kwa idadi kubwa zaidi ya watu duniani, Indonesia, zikiwemo za Rais anayemaliza muda wake Joko Widodo, zimedaiwa kuvujishwa na kuuzwa. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na vyombo vya habari jana Alkhamisi.

Jakarta Globe imeripoti kuwa, mamilioni ya nambari za utambulisho za walipa kodi "zimeuzwa kwa $10,000 kwenye tovuti iitwayo Breach Forum, ambayo ni akaunti inayodaiwa kumilikiwa na mdukuzi anayejulikana kama Bjorka. Kwa mujibu tovuti hiyo ya habari, uuzaji wa taarifa za watu hao ulikamilika siku ya Jumatano.

342/