Waandamanaji hao ambao ni wafanyakazi wa taasisi mbalimbali za Umoja wa Ulaya, walikuwa wamebeba mabango yenye maandishi: "Wafanyakazi wa EU wanaunga mkono amani na haki" wakipinga sera ya Umoja wa Ulaya kuhusu maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu na Israel.
Vilevile wametoa wito wa kulaaniwa jinai zote na ukiukaji wa haki za binadamu unaofanywa na Israel katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu, kusitishwa biashara ya silaha kati ya nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya na Israel, na kufutwa makubaliano yote kati ya EU na serikali ya Tel Aviv.Wafanyakazi wa taasisi mbalimbali za Umoja wa Ulaya pia wametaka kutekelezwa maamuzi ya hivi karibuni ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ambayo imeishutumu Israel kwa kufanya mauaji ya kimbari kutokana na mashambulizi yake ya mara kwa mara kwenye ukanda wa Gaza.
Ni vyema kueleza kuwa, aghlabu ya nchi za Magharibi zinashirikiana na Israel kwa njia moja au nyingine katika mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala huo katili dhidi ya raia wa Palestina katika eneo la Ukanda wa Gaza.
342/