"Aidah Taleb", Mtafiti na Mwalimu wa Sayansi ya Kidini kutoka Lebanon, alisema katika mahojiano na mwandishi wa habari ABNA:
Kwa mujibu wa Aya ya 200 ya Qur'an Tukufu katika Surat Al-Imran:
«يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اصْبِرُوا وَصَابِرُوا وَرَابِطُوا وَاتَّقُوا اللَّهَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ»
"Enyi mlio amini! Kuweni na subira, na himizaneni kusubiri (na kuvumilia) na kuweni macho, na mcheni Mwenyezi Mungu, ili mpate kufanikiwa".
Swali liko hapa: Ni jinsi gani tunatakiwa kusubiri?! Ikiwa tumekaa na kufunga mikono yetu, hilo litakuwa na maana kwamba tumesubiri?!.
Akaongeza kusema: Subira maana yake ni nguvu, uwezo, jihadi na kufanya vitendo, na ikiwa hatuko hivyo, vipi itaitwa subira?!.
Mikutano kama 'Mkutano wa Umoja wa Kiislamu' huwapa watu wenye subira nguvu nyingi, na kuleta nguvu na uwezo kwa watu. Kwa hiyo, tunawaambia (na kuwahimiza) ndugu zetu kusimama imara dhidi ya uvimbe huu wa Saratani wa Israel na Amerika.
Taleb alisema: Maadui wanasema "sisi (yaani: wao) ni uti wa mgongo wa dunia" na wanaisaidia Israel, lakini (Sisi Waislamu) tuna nguvu kubwa na lazima tuuvunje uti huu wa mgongo, lazima tufanye hivi kwa irada, nguvu, subira, na kwa kuchunga vitendo vya adui.
Alifafanua akisema: Sote lazima tuwe waangalifu, yaani, tuwe waangalifu juu ya matendo ya adui, tuwasiliane sisi kwa sisi, na tuwe imara na thabiti katika misimamo yetu ya kijeshi na jihadi.