Katika taarifa tofauti Hizbullah ya Lebanon imetangaza kuwa, imetekeleza operesheni tano mpya dhidi ya ngome na malengo ya utawala wa Kizayuni. Hizbullah imeeleza katika taarifa yake kwamba, sambamba na kuwaunga mkono wananchi wa Palestina huko Gaza na muqawama wao wa kijasiri na wa heshima, wapiganaji hao wa muqawama walilenga kwa kombora kambi ya "Al-Baghdadi" (kitongoji cha Al-Baghdadi kaskazini mwa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu) ya jeshi la kibaguzi la Israel.
Imekuja katika taarifa hiyo kuwa, shambulio la makombora dhidi ya kituo cha "Ma'ayan Baruch", shambulio dhidi ya makao makuu ya rada katika mashamba ya Sheba yanayokaliwa mabavu (kusini mwa Lebanon), kufuatilia nyendo na kuwalenga shabaha askari wa utawala wa Kizayuni katika eneo la "Jal al-Alam ni miongoni mwa zilizokuwa operesheni nyingine za Hizbullah ya Lebanon.
Makombora ya Fadi-1 na Fadi-2 ya Hizbullah ya Lebanon nayo pia siku ya Jumatatu yaliingia kwenye medani ya vita kwa mara ya kwanza. Lengo lilikuwa ni kulenga kituo kikubwa zaidi na uwanja wa ndege wa Jeshi la Anga la Israel kusini mashariki mwa Haifa katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu. Mifumo ya kuzuia makombora wa utawala wa Kizayuni haikufanya lolote, na makombora ya Hizbullah yalifika kwenye kituo nyeti cha anga cha Ramat David kwa uwezo mkubwa wa kulipuka.
Vikosi vya muqawama wa Kiislamu vya Iraq pia vimetangaza kwa kuchapisha taarifa isemayo: Katika kuendeleza utendajii wa kimuqawama dhidi ya uvamizi wa Wazayuni na katika kuunga mkono wananchi wa Palestina na kukabiliana na mauaji ya raia wakiwemo watoto na wanawake yanayofanywa na utawala ghasibu wa Kizayuni, ndege isiyo na rubani ya "Al-Arfad" imelenga shabaha katika Bonde la Jordan katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na Israel.
Muqawama wa Kiislamu umesisitiza kuwa operesheni ya kuangamiza ngome za adui inaendelea kwa kasi kubwa.
Sayyid Hassan Nasrallah, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon alisisitiza baada ya hatua ya kigaidi ya utawala wa Kizayuni katika mlipuko wa pager na vyombo vya mawasiliano na kusababisha kuuawa shahidi na kujeruhiwa maelfu ya watu, kwamba; ukweli ni kwamba adui mzayuni ana uwezo wa kiteknolojia kwa kuegemea Magharibi na hilo ni jambo lisilopingika; lakini nasema kwa uhakika kamili kwamba pigo hili halitatufanya tutoke kwenye njia yetu ya mapambano na badala yake tutasimama kidete kwa nguvu zote dhidi yao.
Kwa hakika, utendaji mpya wa Hizbullah ya Lebanon katika kuendelea na upanuzi wa operesheni zake kaskazini mwa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu unaonyesha azma ya vikosi vya muqawama ya kusimama kidete kukabiliana na utawala wa Kizayuni na waungaji mkono wao wa Kimagharibi. Kwa kuchukua wigo mpana operesheni za Hizbullah ya Lebanon kivitendo maeneo ya kaskazini ya ardhi zilizokaliwa kwa mabavu (Israel) ambako maelfu ya Wazayuni waliishi katika vitongoji haramu, yamekuwa hayakaliki tena na Wazayuni hao wanalazimika kuyakimbia maeneo hayo.
Katika upande mwingine, maandamano katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu pia yanaendelea dhidi ya Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni, Benjamin Netanyahu na familia za mateka wa Kizayuni zinamtuhumu kwa kushindwa kwake kufanya mazungumzo ya kusitisha vita na HAMAS na hivyo kufungua njia ya kuachiliwa huru mateka hao.
inai za kinyama za Wazayuni kupitia operesheni kubwa za kigaidi nchini Lebanon na kuuawa shahidi raia wa Lebanon, kwa mara nyingine tena zimedhihirisha dhati na unyama wa Wazayuni kwa walimwengu na kuonesha kuwa, utawala wa Kizayuni unaendelea na ugaidi wake ulioratibiwa.
Operesheni za kigaidi nchini Lebanon, kinyume na matakwa na tathmini ya Wazayuni, hazikufanikiwa kufikia malengo yake machafu na badala yake zimeleta mshikamano mkubwa mbele ya muqawama na ushirikiano imara zaidi wa kambi ya muqawanma sambamba na uungaji mkono wa wananchi wa Lebanon na eneo hili kwa Hizbullah na kambi ya muqawama kwa minajili ya kuendelea kukabiliana na utawala wa Kizayuni wa Israel.
342/