Main Title

source : Parstoday
Jumanne

24 Septemba 2024

16:25:48
1488170

Profesa Fraihat: Vita vya Lebanon ni vya tatu vinavyofadhiliwa na serikali ya Biden

Ibrahim Fraihat, Profesa wa Taaluma ya Usuluhishi wa Mizozo ya Kimataifa katika Taasisi ya Doha ya Mafunzo ya Wahitimu, amesema kupanuka kwa vita vilivyoanzishwa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Ukanda wa Ghaza hadi Lebanon kulitarajiwa, lakini kile ambacho hakikutarajiwa ni idadi kubwa ya vifo ndani ya muda wa siku moja.

Profesa Fraihat amebainisha hilo akisema: "karibu raia 500 wameuawa kwa siku moja. La kushangaza zaidi ni ukimya wa serikali za Magharibi. Hakujawa na matamshi ya maana na wala hakuna shinikizo la kweli kwa serikali ya Israel kusitisha mashambulizi yake".

Akizungumza katika mahojiano na televisheni ya Aljazeera, Fraihat ameeleza bayana kwamba Rais wa Marekani Joe Biden ndiye anayefadhili vita hivyo.

Mhadhiri huyo wa chuo kikuu amelifafanua hilo kwa kusema: "hivi ni vita vya tatu vilivyofadhiliwa na Marekani wakati wa urais wake baada ya Ukraine na Ghaza. Anatuma wanajeshi zaidi na silaha zaidi kwa Israel, kwa hivyo vitendo vyenyewe vinajieleza”.

 Profesa Fraihat ameendelea kueleza kwamba, vita vya Lebanon vimetokana na kushindwa Biden huko Ghaza "kwa sababu amekuwa akiiunga mkono Israel huko na kuihamasisha". Halikadhalika, amesema waziri wake wa mambo ya nje, Antony Blinken, hakufanikiwa chochote wakati wa ziara zake saba katika eneo hili hata kwa kufanikisha kubadilishana mateka; na akaongeza kuwa hakuna ajuaye, huenda kuna vita vya nne vitakuja kabla ya Joe Biden kuondoka madarakani.../

342/