Main Title

source : Abna
Alhamisi

26 Septemba 2024

01:36:46
1488547

Ujumbe wa Ayatollah Makarim Shirazi kwa Sayyid Hassan Nasrullah:

Upinzani (Muqawamah) wako dhidi ya mstari wa mbele wa jeshi la ukafiri na na bandia ni wa kupigiwa mfano na wa kusifiwa

Ayatollah al-Udhma Makarim Shirazi amesisitiza katika ujumbe wake kwa Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Hezbollah ya Lebanon ambapo amesema: Uungaji mkono wa Uislamu na Waislamu na Upinzani wenu wapendwa dhidi ya mstari wa mbele wa jeshi la ukafiri na bandia (lililozuka); ni wa kupigiwa mfano na wa kusifiwa, na ahadi ya Mwenyezi Mungu isemayo: "وَلَيَنْصُرَنَّ اللهُ مَنْ يَنْصُرُهُ" "Na hakika Mwenyezi Mungu atawanusuru (atawasaidia) wale wanao mnusuru (wanao msaidia)". [Surat al-Haj: Aya ya 40]

Ni kwa ajili yenu / ni kwa haki enyi Mujahidina na watu wa Mapambano ya Upinzani (Muqawamah) na wastahimilivu, na mnaodhulumiwa wa ardhi hiyo, na hiyo ni ahadi ya kweli itakayotimia.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul_Bayt (a.s) - ABNA - Ayatollah al-Udhma Makarim Shirazi alisisitiza katika ujumbe wake kwa Katibu Mkuu wa Hezbollah nchini Lebanon kwa kusema:

Uungaji mkono wa Uislamu na Waislamu na upinzani wako dhidi ya mstari wa mbele wa jeshi la ukafiri na bandia, ni wa kupigiwa mfano na wa kusifiwa, na ahadi isemayo:

 "وَلَيَنْصُرَنَّ اللَّهُ مَنْ يَنْصُرُهُ"

"Na hakika Mwenyezi Mungu atawanusuru (atawasaidia) wale wanao mnusuru (wanao msaidia)".

[Surat al-Haj: Aya ya 40]

_

 Ni ahadi ya kweli itakayotimia kwenu enyi Mujahidina na wana Mapambano ya Muqawamah (Upinzani) na mnaodhulumiwa katika ardhi hiyo.

Andiko / Nakala ya ujumbe huo wa Marjii huyu mkubwa ni hii kama ifuatavyo:

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu.

Kwako ewe Mwanachuoni na Mujahidina, Ndugu Hujjatul-Islam Wal-Muslimina, Sayyid Hasan Nasrullah (Mwenyezi Mungu akuhifadhi na azidishe mafanikio yako).

Ndugu Katibu Mkuu wa Hezbollah ya Lebanon

Assalamu Alaikum

Habari za uadui na uvamizi wa utawala wa Kizayuni unaochukiwa katika ardhi ya Lebanon, na umwagaji damu za watu madhulumu na kuuawa Shahidi idadi kubwa ya Wanawake na Watoto wasio na hatia, na watu wasio na ulinzi (himaya), na pia idadi ya Wanazuoni na Wasomi na Makamanda na Wapiganaji wa ardhi hiyo, zimesababisha maumivu makubwa nyoyoni na wasiwasi.

Baada ya miezi kadhaa ya jinai huko Gaza (Palestina), utawala bandia (na wa kuzuia) wa Israel na viongozi wake wenye unyama na vichaa, katika kivuli cha (sapoti ya) ukimya wa wadai Haki za Binadamu na Uhuru na Taasisi za Kimataifa, unaendelea na jinai zake kila siku bila kuwa na woga, na sasa wana hamu ya kuvamia ardhi za nchi zingine.

Serikali za Kiislamu zinapaswa kujua kwamba ikiwa moto huu (wa vita) hautazimwa na mbwa huyu (Israel) mwenye kichaa hatozuiliwa, basi cheche za moto wake zitateketeza Umma mzima wa Kiislamu, na utaathiriwa na Saratani (Israel) hii ya Kimataifa.

Bila shaka, imekuwa hivyo siku zote, kwamba wakati wowote dhuluma inapofikia kilele chake, ndio hukaribia mwisho wake, na Sunna ya Mwenyezi Mungu ya kuwaangamiza na kuwatokomeza waharibifu hao itajiri juu yao, Insha Allah.

Ushindi wa Uislamu na Waislamu na upinzani wenu dhidi ya mstari wa mbele wa jeshi la (mkondo wa) ukafiri na bandia (likiwa kama jeshi la Taifa bandia lililozushwa Mashariki ya Kati), ni wa kupigiwa mfano na kusifiwa, na ahadi isemayo:

“Na Hakika Mwenyezi Mungu atawanusuru (atawasaidia) wanaonusuru(wanao msaidia)”

Ni ahadi ya kweli itakayotimia kwenu enyi Mujahidina na watu wa Mapambano ya Muqawamah (Upinzani) na mnaodhulumiwa katika ardhi hiyo, na ushindi wenu wa mwisho kabisa na kamilifu kwa msaada wa Mwenyezi Mungu, utashuhudiwa na Ulimwengu na Walimwengu.

Ni lazima kwa Waumini na Waislamu wote wasipuuze na kughafilika na suala la kuomba Dua njema ya kheri kwa Mwenyezi Mungu na kufanya Tawassul kwa Watakasifu na Watoharifu (Amani iwe juu yao), kwa ajili ya kuwaangamiza waovu na wakandamizaji na madhalimu, na kusaidia Mapambano ya Upinzani kwa njia yoyote ile iwezekanayo, ya kimaada na kimaanawi.